06. Sababu ya tano ya maisha mazuri: Kumtaja Allaah kwa wingi

5- Miongoni mwa sababu kubwa za kukifungua kifua na kukifanya kuwa na utulivu ni kumtaja Allaah kwa wingi. Hakika kitendo hicho kina athari kubwa ya kukifungua kifua na kukituliza na pia kuondosha msongo wa mawazo na misononeko yake. Amesema (Ta´ala):

أَلَا بِذِكْرِ اللَّـهِ تَطْمَئِنُّ الْقُلُوبُ

“Zindukeni! Kwa kumtaja Allaah nyoyo hutulia!”[1]

Kumtaja Allaah kuna athari kubwa ya kufikia malengo haya kwa njia yake ya kipekee na pia kutokana na zile thawabu na ujira ambao mja anataraji.

[1] 13:28

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdur-Rahmaan bin Naaswir as-Sa´diy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Wasaa-il-ul-Mufiydah lil-Hayaat-is-Sa´iydah, uk. 21
  • Imechapishwa: 10/06/2020