Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) amesema:

 وَإِذْ قَالَ رَبُّكَ لِلْمَلَائِكَةِ إِنِّي جَاعِلٌ فِي الْأَرْضِ خَلِيفَةً ۖ قَالُوا أَتَجْعَلُ فِيهَا مَن يُفْسِدُ فِيهَا وَيَسْفِكُ الدِّمَاءَ وَنَحْنُ نُسَبِّحُ بِحَمْدِكَ وَنُقَدِّسُ لَكَ ۖ قَالَ إِنِّي أَعْلَمُ مَا لَا تَعْلَمُونَ

“Pindi Mola wako alipowaambia Malaika: “Hakika Mimi nitaweka katika ardhi khalifa.” Wakasema: “Utaweka  humo atakayefanya uharibifu ndani yake na kumwaga damu na ilihali sisi tunakusabihi na tunakutukuza?” Akasema: “Hakika Mimi nayajua zaidi yale msiyoyajua.”[1]

Hapa kunatajwa fadhilah za Aadam (´alayhis-Salaam), ambaye ndiye baba wa watu, kwamba Allaah alipotaka kumuumba aliwaeleza Malaika juu ya hilo na kwamba Allaah atamfanya kuwa ni khalifa ardhini. Ndipo Malaika (´alayhimus-Salaam) wakasema:

أَتَجْعَلُ فِيهَا مَن يُفْسِدُ فِيهَا

“Utaweka  humo atakayefanya uharibifu ndani yake… ”

Kwa maasi.

وَيَسْفِكُ الدِّمَاءَ

“… na kumwaga damu.”

Hapa kuna kufanywa maalum jambo lenyewe baada ya kulitaja kwa jumla kwa ajili ya kubainisha ubaya wa mauaji. Huku ni kwa kudhania kwao tu kwamba khalifa huyu atakayewekwa ardhini kutazuka kutoka kwake mambo hayo. Ndip Mwanzilishi viumbe akamtaka kutokamana, akamtukuza na akaeleza kwamba atatekeleza ´ibaadah ya Allaah kwa njia iliyosalimika kutokamana na maharibifu. Maneno yao:

وَنَحْنُ نُسَبِّحُ بِحَمْدِكَ

“… ilihali sisi tunakusabihi… “

Bi maana tunakutakasa matakaso yanayolingana na himdi na utukufu Wako.

وَنُقَدِّسُ لَكَ

“…tunakutukuza… “

Kuna uwezekano maana yake ikawa: tunakutukuza na kukutakasia nia Wewe pekee na pia maana yake inaweza kuwa tunakutwahirisha kwa tabia nzuri, kama mfano wa kumpenda, kumnyenyekea na kumuadhimisha Allaah. Tunaitwahirisha kutokamana na tabia mbaya. Allaah (Ta´ala) akasema kuwaambia Malaika:

إِنِّي أَعْلَمُ

“Hakika Mimi nayajua zaidi… “

Yanayohusiana na huyu khalifa.

مَا لَا تَعْلَمُونَ

“… yale msiyoyajua.”

Kwa sababu maneno yenu ni kutokana na vile mlivyofikiria. Mimi najua yenye kuonekana waziwazi na yaliyofichikana na najua zaidi kwamba kuna kheri nyingi kabisa zitapatikana kwa kumuumba khalifa huyu kuliko shari mnayodhania. Ingelitosha kama kusingelikuwa kheri nyingine zaidi ya kwamba Allaah ametaka kuteua kutoka kwao Manabii, Mitume, wakweli, mashahidi, waja wema, kudhihiri alama Zake juu ya viumbe, kupatikana ufanyaji wa ´ibaadah ambao usingelipatikana endapo asingemuumba khalifa  huyu – kama mfano wa jihaad na nyenginezo – na pia kupate kudhihiri sura ya mwanadamu hatua kwa hatua kwa kheri na shari baada ya majaribio, abainike adui kutokamana na mpenzi Wake, kundi lake kutokamana na wenye kumpiga vita na pia ipate kudhihiri sura ya Ibliys hatua kwa hatua kwa shari alionayo na akasifika kwazo. Hizi ni hekima kubwa ambapo baadhi tu zinatosheleza juu ya hilo.

[1] 02:30

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdur-Rahmaan bin Naaswir as-Sa´diy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Taysiyr-ul-Kariym, uk. 38
  • Imechapishwa: 10/06/2020