Ibn ´Uthaymiyn kuhusu kufaidika kutoka kwa Ahl-ul-Bid´ah

Swali: Mtu anatakiwa kuchukua msimamo gani ikiwa mtu yuko na baadhi ya makosa ni mamoja ni makosa ya ´Aqiydah au mengine lakini hata hivyo anazo kheri nyingi na ni vipi mtu atachuma faida kutoka kwake akiwa ni mwandishi mzuri au ni mtu muhimu au anao ujuzi ambao wengine hawana?

Jibu: Ikiwa mtu huyu anaweka wazi Bid´ah alizonazo, basi haitakiwi kwa mtu kuchukua chochote kutoka kwake. Mtu asende kwake. Ijapokuwa haathiriki naye,  atawaghuri wengine. Hiyo ina maana kwamba watu watadanganyika naye na watadhania kwamba mzushi huyu yuko katika haki. Kwa ajili hiyo mtu hatakiwi kwenda kwa Ahl-ul-Bid´ah pasi na kujali mali au elimu kiasi gani anayofaidika kutoka kwake. Kwa sababu jambo hilo linawaghuri wengine.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Liqaa’ al-Baab al-Maftuuh (58 A)
  • Imechapishwa: 02/09/2021