Ibn ´Uthaymiyn kuhusu kucheza kikoba/kibati

Swali: Sisi ni marafiki ambao tunataka kucheza kikoba ambapo kila mmoja wetu anatoa pesa kiwango fulani kama vile 4.000 kisha pesa hizo zinapokelewa na mmoja katika sisi na tunaendelea na mpangilio huo mpaka anapofikia mtu wa mwisho. Sababu ya kukuuliza ni kwa kuwa tumesikia kuwa ni haramu au kwamba ni jambo lina utata ndani yake. Ni ipi fatwa yako juu ya masuala haya?

Jibu: Fatwa yangu juu ya masuala haya ni kwamba yanafaa. Hakuna utata wowote kabisa. Bali ni katika kusaidizana kati ya waislamu. Kwa mfano wakiwa watu kumi na wakaelewana kila mmoja katika wao atoe pesa 1.000 kwa mwezi na apewe mmoja wao. Mwezi wa pili akapokea mtu wa pili. Mwezi wa tatu akapokea mtu wa tatu na kwendelea mbele mpaka akarudiliwa yule wa kwanza upya. Kuna madhara gani ya kufanya hivo? Hapa ribaa iko wapi? Ni kheri na kusaidiana. Wakati fulani mtu anakuwa katika hali ngumu na mshahara anaopata haumtoshi. Hivyo anawataka msaada ndugu zake na anawaambia wamkope. Ikiwa mtu atasema kwamba atapohitajia kukopwa basi atakopwa. Je, amechukua ziada? Hapana, hakuchukua ziada. Amechangia 1.000 na amepokea zilezile 1.000. Hazikuzidi.  Hakuna utatizi katika hili.

Kutoa fatwa kwamba ni haramu ni makosa. Kila mkopo ambao anafaidika yule mwenye kukopa basi hiyo ni ribaa. Hapa ni pale ambapo kunufaika ni kwa kuongezwa au manufaa kwa mfano mtu anamkopesha mwingine 1.000 kwa sharti akae kwenye nyumba yake mwaka mmoja. Ama katika hali hii yule mwenye kukopa hakupokea ziada ya kile alichotoa. Yeye amenufaika na ndugu zake nao pia wamefaidika. Mimi ninavoona ni kwamba ni jambo halina tatizo na ni katika kusaidiana kati ya ndugu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (58) http://binothaimeen.net/content/1322
  • Imechapishwa: 03/11/2019