Ibn ´Uthaymiyn kuhusiana na kanda ambazo wanafunzi wanachapana wao kwa wao

Swali: Yapi maoni yako kusambaza kanda/kaseti ambazo wanafunzi wanafanyiana Rudduud wao kwa wao?

Jibu: Naona kuwa kanda ambazo zinahusiana na kurusha na mwingine anarudisha ambazo uhakika wa mambo ukizingatia utaona kuwa msingi wake ni magomvi tu, naona kuwa zisisambazwe. Kwa kuwa zinapelekea kuwadangana wasikilizaji na kuwagawa kwenye makundi. Ama ikiwa ni Radd ambayo ni lazima, kwa mfano mtu ambaye anasambaza upotofu wake katika kaseti na hakuna budi ila kubainisha, hii ni lazima kuisambaza. Lazima Radd hiyo isambazwe. Mtu atalijua hilo huwa akijua kwa viashirio kama kile kinachosambazwa baina ya watu ni ugomvi tu au kama [lengo] ni kubainisha haki. Ikiwa lengo ni kubainisha haki basi ni lazima zisambazwe, na kama ni ugomvi tu zisisambazwe. Kwa kuwa watu kwa hakika wako na haja kubwa ya kitu kitachowafanya kuwa wamoja na si   kitu kitachowafarakisha. Na kama mnavyojua wenyewe vijana hawaelewi mambo kama inavyowapasa. Huenda akadanganyika mmoja wao na hili na mwingine na  lile. Hatimaye kukatokea fitina.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Liqaa’ al-Baab al-Maftuuh (60 A)
  • Imechapishwa: 02/09/2018