Ibn ´Uthaymiyn kubeba msahafu katika swalah za faradhi

Swali: Ni ipi hukumu ya kutazama ndani ya msahafu katika swalah ya faradhi na swalah ya sunnah? Ni ipi hukumu ya kusoma baadhi ya du´aa, kama du´aa ya Istikhaarah, katika swalah ya sunnah?

Jibu: Kusoma ndani ya msahafu katika swalah za faradhi na swalah za sunnah, ikiwa anaweza kusoma bila kufanya hivo ndio bora zaidi. Kwa sababu kusoma ndani ya msahafu kunahitajia kutazama, kubeba msahafu, kuuweka chini na kufungua karatasi. Kote huku ni kutikisika. Ikiwa mtu amelazimika kusoma ndani yake hakuna neno. Ni mamoja katika swalah ya faradhi na swalah ya sunnah. Miongoni mwa hayo yanayohusiana na swalah ya faradhi ni kwamba baadhi ya watu katika Fajr ya siku ya ijumaa hawakuhifadhi Suurah “as-Sajdah” wala “al-Insaan”. Hivyo baadhi ya watu wanaiacha sunnah hii kwa sababu hawakuhifadhi. Tunawaambia kwamba mambo ni mapana. Ikiwa hukuhifadhi moyoni basi zisome ndani ya msahafu. Hakuna neno kufany hivo. Mama wa waumini ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) katika swalah zake za Tahajjud alikuwa akisoma ndani ya msahafu. Kwa hivyo hakuna neno. Lakini akiwa hana haja ya kusoma ndani ya msahafu basi asifanye hivo.

Kwa mnasaba huu napenda kuzindua kitu ambacho watu walikuwa wakikifanya halafu wakakipunguza na himdi zote anastahiki Allaah. Kitu chenyewe ni kwamba baadhi ya maimamu katika Tarawiyh au Tahajjud Ramadhaan wanachukua msahafu ili kumfuata imamu. Hili ni kosa. Kwa sababu kitendo hichi kinapelekea mtu kufanya harakati zisizohitajika. Jengine ni kwamba kitendo hichi kinamzuia mswaliji kuweka mikono juu ya kifua chake. Pengine vilevile akatupa mazingatio ya kumsikiliza imamu kwa kule kutazama kwake Aayah ndani ya msahafu.

Ikiwa imamu hakuhifadhi vizuri ambapo akawaambia baadhi ya waswaliji waswali nyuma yake na anapokosea basi wamrekebishe. Hili halina neno. Ndani kuna manufaa. Ama kumfuata tu haifai.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (58) http://binothaimeen.net/content/1331
  • Imechapishwa: 10/11/2019