Ibn ´Uthaymiyn kazi ambayo mtu kapasi kwa kughushi

Swali: Mimi nimetakharuji kwenye chuo kikuu lakini kwa kughushi. Nimepeleka vyeti vyangu kwenye idara fulani ili kupata kazi. Ni ipi hukumu ya mshara wangu kutokana na hali niliyokutajia?

Jibu: Ninaonelea kuwa endapo kufaulu kwa kughushi itakuwa inahusiana na kile cheti cha mwisho ambacho mshahara umejengeka juu yake kwamba hastahiki mshahara ule. Kwa sababu kilichojengeka juu ya batili nacho pia ni batili. Kutokana na hili naona kuwa anatakiwa kurudi kwa mara ya pili kufanya tena mtihani. Isipokuwa tu ikiwa kama kazi hiyo imejengwa juu ya yale masomo aliyopasi kwayo. Katika hali hiyo naonelea kuwa hakuna neno. Lakini hata hivyo itamlazimu kutubia. Mfano wa hilo ni kama ameteuliwa kufanya kazi ya hesabu ambapo katika masomo ya hesabu alipasi na akaghushi katika masomo mengine, natarajia kuwa kazi yake hii itakuwa ni halali. Kwa sababu ameimarisha kazi yake hii maalum aliyosomea. Pamoja na hivyo itamlazimu kutubia kwa Allaah kutokana na ghushi aliyofanya.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (01)
  • Imechapishwa: 09/09/2020