Kipindi cha mwisho kumeenea vipeperushi vinavyotoka nje ya nchi na heunda vikawa vinaandikwa ndani ya nchi. Ndani yake wanatukanywa na kuwaponda watawala. Ndani yake hakutajwi sifa moja miongoni mwa sifa za kheri ambazo wanafanya. Hapana shaka kwamba kufanya hivi ni kusengenya. Mambo yakishakuwa hivo kwamba ni usengenyi basi kuvisoma ni haramu. Kadhalika kuvisambaza ni haramu. Haijuzu kuvieneza na kuvisambaza kati ya watu. Kwa yule atakayeviona basi avichanechane au avichome. Kwa sababu vipeperushi hivi vinasababisha fitina, vinasababisha vurugu na vinasababisha shari.

Muftiy wa nchi hii ya Saudi Arabia, Shaykh wetu ´Abdul-´Aziyz bin Baaz (Allaah amuwafikishe na amrehemu duniani na Aakhirah) ametahadharisha kueneza vipeperushi hivi[1], amebainisha kuwa vinasababisha fitina kubwa na vinasababisha kufarikisha kati ya watawala na raia. Vipeperushi hivo ni sababu ya shari na ufisadi na amevitahadharisha – Allaah amuwafikishe kwa yale yaliyo na kheri. Ametadharisha kueneza vijikaratasi hivi vinavyoenea. Kadhalika mimi pia natahadharisha pamoja naye na vivyo hivyo ndugu zetu wengine wanachuoni wanaowatakia watu mema wanatahadharisha Ummah wao juu ya kueneza vipeperushi hivi. Mimi nawaambieni: Je, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakusema kuhusu usengenyi:

“Hakika ni kule kumsema ndugu yako kwa anayoyachukia”?

Vipeperushi hivi si anavichukia mtawala ambaye kumeenezwa yanayosemwa juu yake? Je, wao wanayachukia mambo hayo? Hapana shaka kwamba wanayachukia.

Mambo yakishathibiti kwamba ni katika usengenyi basi itambulike kuwa kusengenya ni miongoni mwa madhambi makubwa. Ni kitu kisichosameheka kwa kuswali, kutoa swadaqah wala kufunga. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Swalah vipindi vitano, ijumaa mpaka ijumaaa nyingine na Ramadhaan mpaka Ramadhaan nyingine ni vyenye kufuta yaliyo baina yake muda wa kuwa mtu atajiepusha na madhambi makubwa.”

Katika tamko lingine imekuja:

“Mtu akijiepusha na madhambi makubwa.”[2]

Kujengea juu ya haya swalah ni zenye kufuta madhambi. Kukiwa kati yake madhambi makubwa hayafutwi. Hivyo basi, mcheni Allaah enyi waja wa Allaah.

Hakika mimi nakariri nasema tena ya kwamba haijuzu kueneza vipeperushi hivi. Yule mwenye kuvieneza anapata dhambi na atapata adhabu yake siku ya Qiyaamah. Ataulizwa juu ya kueneza kasoro za viumbe na kasoro za watawala. Pamoja na kwamba baadhi ya vipeperushi hivi vimekusanya kati ya usengenyi na uongo. Kwa msemo mwingine ndani yake yapo mambo ambayo hayakuthibiti kabisa.

Tunamuomba Allaah (Ta´ala) awalinde wananchi wetu na watawala wetu kutokamana na maharibiko, ajaalie vitimbi vya wenye kueneza ufisadi kwenye shingo zao na aangamize yale wanayoyafanyia mikakati juu ya nchi hii yenye amani.

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/ibn-baaz-kuhusu-ibn-laadin-al-faqiyh-och-al-masariy/

[2] Muslim (233).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ´Ulamaa-ul-Kibaar fiy al-Irhaab wat-Tadmiyr, uk. 458-459
  • Imechapishwa: 09/04/2020