Ibn Baaz kuhusu Ibn Laadin, al-Faqiyh na al-Mas´ariy

Vipeperushi hivi vinavyotoka kwa al-Faqiyh, al-Mas´ariy au mtu mwengine katika walinganiaji wa batili na walinganiaji wa shari, ni lazima kuviharibu, kuvichana na kuvipuuza. Ni lazima kwa yule mwenye kuweza awanasihi, kuwaongoza katika haki na kuwatahadharisha na batili. Haijuzu kwa yeyote kushirikiana nao katika shari hii. Ni lazima wanasihiwe na warudi katika haki. Ni wajibu kwao kuachana na batili hii. Nasaha yangu kwa al-Mas´ariy, al-Faqiyh, Ibn Laadin na wengine wote wanaopita katika mfumo wao, wajiweke mbali na njia hii mbaya na badala yake wamche Allaah kwa yale waliyofanya hapo kabla.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=7bDJjr7dAVs
  • Imechapishwa: 09/04/2020