Ibn Baaz kuhusu zakaah juu dhahabu za kujipamba

Swali: Dhahabu zinazotumiwa kwa ajili ya kujipamba na mfano wake ni wajibu kuzitolea Zakaah?

Jibu: Kauli sahihi ni kwamba zinatolewa Zakaah. Kuna tofauti kwa wanachuoni. Baadhi ya wanachuoni wanaonelea kuwa zinazotumiwa hazitolewi Zakaah. Lakini hata hivyo kauli sahihi ni kwamba zinatolewa Zakaah kutokana na ujumla wa dalili.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=14490
  • Imechapishwa: 23/11/2014