Swali: Kuna Fatwa nimesoma katika baraza la kufutu lililo Jordan ya kwamba Talaka haipiti pindi mke anapokuwa sio mtwaharifu [yumo katika hedhi]. Nikawa sikujali nikamtaliki kwa kumkhofisha na huku mimi najua kuwa Talaka haipiti kutokana na Fatwa hii. Ni ipi hukumu?
Jibu: Talaka kwa mwenye hedhi haijuzu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimkataza Ibn ´Umar pindi alipomtaliki mke wake katika hedhi. Alimkataza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na akamghadhibikia na akamuamrisha abaki nae mpaka atwaharike, kisha apate hedhi tena kisha atwaharike, kisha apate hedhi tena kisha atwaharike, kisha baada ya hapo akipenda amtaliki kabla ya kumwingilia. Kisha akasema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Hiyo ndi edda Aliyoamrisha Allaah Kuwataliki wanawake ndani yake.”
Ikiwa katika hedhi au nifasi, haifai kwake kumtaliki. Asubiri mpaka atapotwaharika. Kisha amtaliki kabla ya kumwingilia. Akimtaliki katika hedhi na yeye (mume) anajua kuwa ana hedhi au nifasi – anajua hilo fika – haijuzu. Akimtaliki, (Talaka) haipiti kutokana na kauli sahihi.
Wanachuoni wengi wanaonelea kuwa inapita pamoja na (mume) kupata madhambi. Anapata dhambi na Talaka imepita. Baadhi ya wanachuoni wengine wanaonelea kuwa haipiti pamoja na kupata madhambi. Anapata madhambi na (Talaka) haipiti. Na hii ndio kauli yenye nguvu kutokana na dalili. Ikiwa alikuwa anajua kuwa ana hedhi wakati alimtaliki, haijuzu kwake kumtaliki wakati wa hedhi wala nifasi. Akiazimia Talaka, anatakiwa kusubiri mpaka atapotwaharika, hapo ndipo amtaliki kabla ya kumwingilia. Amtaliki Talaka moja na wala asizidishe hapo. Hii ndio Sunnah.
- Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: http://subulsalam.com/catplay.php?catsmktba=155
- Imechapishwa: 03/05/2015
Swali: Kuna Fatwa nimesoma katika baraza la kufutu lililo Jordan ya kwamba Talaka haipiti pindi mke anapokuwa sio mtwaharifu [yumo katika hedhi]. Nikawa sikujali nikamtaliki kwa kumkhofisha na huku mimi najua kuwa Talaka haipiti kutokana na Fatwa hii. Ni ipi hukumu?
Jibu: Talaka kwa mwenye hedhi haijuzu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimkataza Ibn ´Umar pindi alipomtaliki mke wake katika hedhi. Alimkataza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na akamghadhibikia na akamuamrisha abaki nae mpaka atwaharike, kisha apate hedhi tena kisha atwaharike, kisha apate hedhi tena kisha atwaharike, kisha baada ya hapo akipenda amtaliki kabla ya kumwingilia. Kisha akasema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Hiyo ndi edda Aliyoamrisha Allaah Kuwataliki wanawake ndani yake.”
Ikiwa katika hedhi au nifasi, haifai kwake kumtaliki. Asubiri mpaka atapotwaharika. Kisha amtaliki kabla ya kumwingilia. Akimtaliki katika hedhi na yeye (mume) anajua kuwa ana hedhi au nifasi – anajua hilo fika – haijuzu. Akimtaliki, (Talaka) haipiti kutokana na kauli sahihi.
Wanachuoni wengi wanaonelea kuwa inapita pamoja na (mume) kupata madhambi. Anapata dhambi na Talaka imepita. Baadhi ya wanachuoni wengine wanaonelea kuwa haipiti pamoja na kupata madhambi. Anapata madhambi na (Talaka) haipiti. Na hii ndio kauli yenye nguvu kutokana na dalili. Ikiwa alikuwa anajua kuwa ana hedhi wakati alimtaliki, haijuzu kwake kumtaliki wakati wa hedhi wala nifasi. Akiazimia Talaka, anatakiwa kusubiri mpaka atapotwaharika, hapo ndipo amtaliki kabla ya kumwingilia. Amtaliki Talaka moja na wala asizidishe hapo. Hii ndio Sunnah.
Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: http://subulsalam.com/catplay.php?catsmktba=155
Imechapishwa: 03/05/2015
https://firqatunnajia.com/ibn-baaz-kuhusu-talaka-wakati-wa-hedhi-2__trashed/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)