Ibn Baaz kuhusu Tahniyk kwa mtoto mchanga

Swali: Je, tahniyk si ilikuwa kwa ajili ya kutafuta baraka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?

Jibu: Jambo hilo ni maalum kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Lengo ilikuwa kwa ajili ya kutafuta ile baraka ambayo Allaah ameijaalia kwake. Lakini hapana vibaya kufanya hivo mtoto anapoletwa kwa baba yake ampe jina au kwa ndugu yake mkubwa kwa lengo la heshima.

Swali: Nakusudia tahniyk?

Jibu: Tahniyk ni Sunnah moja kwa moja daima.

Swali: Kwa tende?

Jibu: Kwa tende ambazo mtu atazitafuna na kuziweka mdomoni mwake. Yatafanywa na mama yake, baba yake au mtu mwingine. Yote ni Sunnah; akimpa jina kuanzia ile siku ya kwanza ya kuzaliwa ni Sunnah, na akimpa jina ile siku ya saba ni Sunnah. Yote yamethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Swali: Kumfanyia Tahniyk kwa kumtolea adhaana kwenye sikio la kulia na kumkimia swalah kwenye sikio la kushoto?

Jibu: Hiyo sio tahniyk. Adhaana na iqaamah ni pale wakati wa kumpa jina. Hapana vibaya kufanya hivo. Akifanya ni sawa na asipofanya pia ni sawa.

Swali: Je, ni Sunnah?

Jibu: Kikosi cha wanazuoni kadhaa wanaona inapendeza. Kumepokelewa juu yake Hadiyth isiyokuwa na neno.

Swali: Akimfanyia tahniyk kwa isiyokuwa tende?

Jibu: Sunnah ni kufanya kwa tende.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24002/هل-تحنيك-المولود-سنة-مطلقا-ام-كان-للتبرك
  • Imechapishwa: 17/08/2024