Swali: Ni ipi hukumu ya mwanaume aliyezini na mwanamke kisha akamuoa na baadaye wakapata watoto na wote – yeye, mke wake na watoto – wakatekeleza faradhi ya Hajj? Je, kosa la uzinzi limeondoka kwao kwa kutekeleza faradhi ya Hajj? Ikoje hali ya watoto? Je, wanahesabiwa kuwa ni watoto wa uzinifu ilihali kuzaliwa kwao kulitokea baada ya ndoa kukamilika, yaani hapakuwa na mimba kabla ya ndoa?
Jibu: Yeyote atakayefanya tawbah, basi Allaah humkubalia tawbah yake hata kama ni kabla ya Hajj. Wakifanya tawbah, basi Allaah huwasamehe hata kama ni kabla ya Hajj. Si sharti Hajj ili kosa lifutwe, bali tawbah inatosha. Ikiwa ametubia na akajuta kwa dhati yale aliyoyafanya, basi Allaah (Jalla wa ´Alaa) humkubalia yule anayefanya tawbah. Tawbah hufuta yaliyotangulia kabla yake na Uislamu hufuta yaliyotangulia kabla yake. Hajj ni ziada ya kheri. Tunamuomba Allaah awaongoze.
Mwanafunzi: Je, inasihi kufunga ndoa na mwanamke mzinifu?
Ibn Baaz: Ndoa inasihi ikiwa ametubia. Lazima aonywe na akumbushwe. Akifanya tawbah na akaidhihirisha tawbah yake, basi hapana vibaya.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2267/حكم-من-زنى-بامراة-ثم-تزوج-بها
- Imechapishwa: 09/01/2026
Swali: Ni ipi hukumu ya mwanaume aliyezini na mwanamke kisha akamuoa na baadaye wakapata watoto na wote – yeye, mke wake na watoto – wakatekeleza faradhi ya Hajj? Je, kosa la uzinzi limeondoka kwao kwa kutekeleza faradhi ya Hajj? Ikoje hali ya watoto? Je, wanahesabiwa kuwa ni watoto wa uzinifu ilihali kuzaliwa kwao kulitokea baada ya ndoa kukamilika, yaani hapakuwa na mimba kabla ya ndoa?
Jibu: Yeyote atakayefanya tawbah, basi Allaah humkubalia tawbah yake hata kama ni kabla ya Hajj. Wakifanya tawbah, basi Allaah huwasamehe hata kama ni kabla ya Hajj. Si sharti Hajj ili kosa lifutwe, bali tawbah inatosha. Ikiwa ametubia na akajuta kwa dhati yale aliyoyafanya, basi Allaah (Jalla wa ´Alaa) humkubalia yule anayefanya tawbah. Tawbah hufuta yaliyotangulia kabla yake na Uislamu hufuta yaliyotangulia kabla yake. Hajj ni ziada ya kheri. Tunamuomba Allaah awaongoze.
Mwanafunzi: Je, inasihi kufunga ndoa na mwanamke mzinifu?
Ibn Baaz: Ndoa inasihi ikiwa ametubia. Lazima aonywe na akumbushwe. Akifanya tawbah na akaidhihirisha tawbah yake, basi hapana vibaya.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2267/حكم-من-زنى-بامراة-ثم-تزوج-بها
Imechapishwa: 09/01/2026
https://firqatunnajia.com/ibn-baaz-kuhusu-ndoa-na-waliozini/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket