Ibn Baaz kuhusu mtu aliyetoka na Jamaa´at-ut-Tabliygh na akaswali kwenye msikiti wa kaburi

Swali: Nilifanya khuruuj na Jamaa´at-ut-Tabliygh kwenda India na Pakistan. Tulikuwa tukikusanyika na kuswali kwenye msikiti ambao ndani yake kuna kaburi. Nimesikia kwamba Swalah haisihi ikiswaliwa kwenye msikiti ambao ndani yake kuna kaburi. Ni yapi maoni yako kuhusu swalah yangu na je natakiwa kuirudi? Ipi hukumu ya kutoka pamoja nao katika sehemu kama hizi?

Jibu: Jamaa´at-ut-Tabliygh hawana elimu katika mambo ya ´Aqiydah. Hivyo haijuzu kutoka pamoja nao, isipokuwa kwa mtu ambaye yuko na elimu na maarifa katika ´Aqiydah sahihi ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ili mtu aweza kuwaelekeza na kuwanasihi na kusaidiana pamoja nao katika mema.

Ni watu wa kazi kunapokuja katika matendo, lakini wanahitajia elimu zaidi na wanachuoni watakaowafunza elimu Tawhiyd na Sunnah.

Ama kuhusu swalah kwenye msikiti ambao ndani yake kuna kaburi, Swalah haisihi. Ni wajibu kurudi kuswali swalah alizoswali humo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kasema:

”Laana ya Allaah iwe juu ya mayahudi na manaswara. Wameyafanya makaburi ya Mitume wao kuwa sehemu ya kuswalia.”

Imepokelewa na al-Bukhaariy na Muslim.

Na kasema tena (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Tanabahini! Hakika waliokuwa kabla yenu walikuwa wakiyafanya makaburi ya Mitume wao na watu wao wema kuwa sehemu ya kuswalia. Tanabahini! Msiyafanye makaburi kuwa ni sehemu ya kuswalia. Hakika mimi nawakataza hilo.”

Imepokelewa na Muslim.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://binbaz.org.sa/mat/1984
  • Imechapishwa: 03/09/2020