Ibn Baaz kuhusu mkusanyiko wa pili msikitini II

Swali: Ni ipi hukumu ya mkusanyiko ambao umechelewa, kisha ukafanya swalah ya mkusanyiko nyingine baada ya swalah iliyoswaliwa kwa adhaana pamoja na imamu wa kudumu?

Jibu: Hakuna tatizo katika hilo. Wakija na imamu tayari ameshaswali, wanaanzisha swalah ya mkusanyiko mwingine na kuswali. Mtume alianzisha mkusanyiko mwingine kwa mtu mmoja aliyekuja na swalah ikawa imempita, akawaambia waliokuwepo:

”Ni nani atakayejitolea kwa huyu akaswali pamoja naye?”

Kwa hiyo wakafanya mkusanyiko mwingine. Kwa sababu swalah ya mtu pamoja na mtu mwingine ni kamili zaidi kuliko kuiswali peke yake. Hivyo ikiwa mkusanyiko umempita na akawakuta wengine, basi ataswali nao wote kama mkusanyiko. Imesimuliwa kuwa Anas na Maswahabah wengine walifanya hivyo.

Ama maoni ya baadhi ya wanazuoni wanaosema wasiswali mkusanyiko tena, bali warudi majumbani mwao na kuswali kila mmoja peke yake, si maoni yenye nguvu. Ni dhaifu na yanayoenda kinyume na Sunnah na kinyume na misingi ya Shari´ah.

Swali: Vipi kuhusu anayewahi Tashahhud ya mwisho?

Jibu: Bora ajiunge pamoja nao, hata kama ni katika Tashahhud ya mwisho. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Kile mtachowahi, kiswalini, na kile mlichokosa, kikamilisheni.”

Hivyo wakiwapata katika swalah basi wajiunge pamoja na imamu hata kama ni katika mkusanyiko.

Swali: Vipi ikiwa swalah imerudiwa baada ya swalah ya Fajr katika nyakati zilizokatazwa kuswali?

Jibu: Haijalishi kitu. Ni mamoja iwe Fajr, ´Aswr au swalah nyenginezo. Wakiwapata wanaswali, basi ajiunge pamoja nao. Hilo ndilo bora na ndio Sunnah, hata kama tayari amekwishaswali.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/980/حكم-اقامة-جماعة-ثانية-بالمسجد-بعد-انتهاء-الاولى
  • Imechapishwa: 29/12/2025