Ibn Baaz kuhusu mfungaji kufanya jimaa kwa kusahau

Swali: Vipi kwa mfungaji ambaye amekula hali ya kuwa amesahau?

Jibu: Hakuna kinachomlazimu. Hana kafara wala kulipa.

Swali: Vipi akifanya tendo la ndoa kwa kusahau?

Jibu: Sahihi ni kwamba funga yake ni sahihi. Isitoshe halazimiki kutoa kafara. Baadhi ya wanazuoni wamebagua jimaa. Hata hivyo hakuna dalili juu ya hilo. Kwa ajili hiyo imekuja katika tamko jengine:

”Anayefungua katika Ramadhaan kwa kusahau hakuna juu yake kulipa wala kafara.”

Swali: Vipi nikimuona anakunywa kwa kusahau?

Jibu: Mkumbushe, kwa sababu ni maasi. Ukimuona anayekunywa au anayekula ndani ya swawm yake, mkumbushe na kumwambia kuwa amefunga. Mweleze na umkataze.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24412/حكم-الصاىم-اذا-اكل-او-شرب-او-جامع-ناسيا
  • Imechapishwa: 07/10/2024