Ibn Baaz kuhusu kutumia manukato yenye pombe

Swali: Je, manukato ya kisasa yenye pombe?

Jibu: Manukato ni yale aina zote za harufu nzuri, isipokuwa kama itajulikana kwamba aina fulani ina kileo. Kwa hivyo kilicholewesha kwa wingi wake hata kidogo chake pia ni haramu. Mfano ni manukato aina ya “kalonia” ambayo inalewesha na haifai kutumika kwa sababu ina kitu kinacholewesha. Kwa hiyo inapaswa kuepukwa. Vivyo hivyo yanakatazwa manukato mengine ambayo yana kitu kinacholewesha. Lakini ikiwa ni manukato safi, ni Sunnah kuyatumia. Ni jambo hili limependekezwa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anapenda manukato na akiyatumia. Kwa hivyo ni jambo linalopendekezwa kwa muumini kutumia manukato.

Swali: Je, inafaa kutumia manukato ambayo hayakosi kuwa na kiasi kidogo cha pombe?

Jibu: Kile kinacholewesha kwa wingi hata kidogo chake ni haramu. Ikiwa hicho kidogo kiwango chake kikubwa kinalewesha yamekatazwa. Lakini kama hakileweshi basi hakikatazwi.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24959/حكم-العطورات-الحديثة-التي-فيها-كحول
  • Imechapishwa: 12/01/2025