Kutoka Minaa mchana na kurudi usiku kwa ajili ya kulala

Swali: Baadhi ya watu katika masiku ya Tashriyq huko Minaa wanakwenda mchana Jeddah au Twaaif kisha wanarudi usiku kulala Minaa. Je, inajuzu kufanya hivo?

Jibu: Bora na salama zaidi ni kuacha kufanya hivyo, kwa sababu Mtume Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikaa Minaa. Kuacha kwenda ni salama zaidi. Kilicho wajibu ni kulala Minaa. Hata hivyo hapana vibaya ikiwa mtu atatoka Minaa kwa ajili ya mahitaji. Lakini kukaa Minaa kama alivyokaa Mtume Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahaba ndio bora zaidi.

Swali: Je, kuna chochote kinachowalazimu?

Jibu: Hakuna kitu kinachowalazimu, hapana.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24958/حكم-الخروج-من-منى-نهارا-والرجوع-ليلا-للمبيت
  • Imechapishwa: 12/01/2025