Swali: Ni yapi maoni yako kukaa kwa Mashaykh wa Ashaa´irah na kusoma kwao elimu ya lugha na khaswa kwa kuzingatia kwamba hakuna Mashaykh (wa Ahl-us-Sunnah) ambao wako imara katika fani hii kikamilifu. Ninamaanisha Mashaykh wa Ashaa´irah ambao wanaitakidi I´tiqaad ya Ash´ariyyah lakini na yuko imara katika fani hii kikamilifu.

Jibu: Ikiwa anaficha ´Aqiydah yake na haibainishi, basi mtu afaidike kwake. Ama ikiwa anabainisha ´Aqiydah ya Ashaa´irah mtu asifaidike [kutoka kwake]. Kwa kuwa anaweza kuchukulia ni mazuri anayoyasema na moyo wake ukapotea. Wajibu ni kuwa na uthabiti pamoja na kuendelea kumnasihi. Lakini ikiwa anaificha na habainishi kitu, mtu afaidike kwake katika mambo ya lugha, mirathi au mengineyo. Lakini ikiwa anadhihirisha ´Aqiydah yake anaachwa na kususwa.

Swali: Ina maana mtu asisome hata kwake?

Jibu: Hapana kwa kuwa hilo linaweze kupelekea kukubali yaliyo kwake

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=14576
  • Imechapishwa: 05/05/2015