Ibn Baaz kuhusu kufasiri nafsi ya Allaah kuwa ni dhati

Swali: Je, kuna tatizo katika kufasiri neno nafsi kwa maana ya dhati katika haki ya Allaah (´Azza wa Jall)?

Jibu: Sijui kizuizi chochote kuhusu ya hilo. Linaweza kufasiriwa kuwa dhati na linaweza pia kuwa na maana nyingine maalum zaidi kuliko dhati. Maana inayoonekana katika dalili za Qur-aan na Hadiyth inajumuisha dhati na pia maana nyingine, kama alivyosema (´Azza wa Jall):

تَعْلَمُ مَا فِي نَفْسِي وَلَا أَعْلَمُ مَا فِي نَفْسِكَ

”Unayajua yale yote yaliyomo katika nafsi yangu na wala [mimi] sijui yale yaliyomo katika Nafsi Yako.”[1]

Hii ni kwa namna inavyomstahiki Allaah. Hakuna ajuaye namna ilivyo isipokuwa Yeye tu (´Azza wa Jall).

[1] 5:116

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25299/ما-حكم-تفسير-النفس-لله-عز-وجل-بالذات
  • Imechapishwa: 25/02/2025