Swali: Ni ipi hukumu ya kuapa kwa Mtume, bin-Nabiy?

Jibu: Haijuzu kuapa kwa asiyekuwa Allaah, haijalishi ni nani. Si Mtume wala mwengine yeyote. Anasema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mwenye kutaka kuapa, basi aape kwa Allaah au anyamaze.”

“Msiape kwa baba zenu, mama zenu wala miungu yenu. Wala msiape kwa Allaah isipokuwa muwe ni wakweli.”

“Atakayeapa kwa kitu kisichokuwa Allaah basi amefanya Shirki.”

Ameipokea Imaam Ahmad kwa isnadi Swahiyh, kutoka kwa ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhu).

Amepokea vilevile Abu Daawuud na Tirmidhiy kwa isnadi Swahiyh kutoka kwa Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Atakayeapa kwa asiyekuwa Allaah, basi amefanya kufuru au Shirki.”

Akasema tena (´alayhis-Salaam):

“Atakayeapa kwa amana, basi si katika sisi.”

Makusudio ni kwamba, ni wajibu kuapa kwa Allaah Pekee. Mtu asiape kwa Mtume wala asiyekuwa Mtume, amana, Ka´abah na kadhalika. Kuapiwa inakuwa kwa Allaah Pekee. Anasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mwenye kutaka kuapa, basi aape kwa Allaah au anyamaze.”

Haijuzu kuapa kwa asiyekuwa Allaah yeyote awae.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=12822
  • Imechapishwa: 20/11/2014