Ibn Baaz kuhusu Istiftaah katika Tarawiyh na Dhuhaa

Swali: Imamu akianza kuswali Tarawiyh na nikasoma du´aa ya kufungulia swalah baada ya Takbiyrat-ul-Ihraam, kisha nikaanza kusoma al-Faatihah na Suurah nyingine kutoka ndani ya Qur-aan, akaswali Rak´ah ya pili na kutoa salamu. Kisha akasimama na kuleta Takbiyrat-ul-Ihraam kwa mara ya pili. Je, maamuma asome du´aa ya kufungulia swalah kwa mara nyingine au atosheke na ile ya mwanzo aliyosoma?

Jibu: Atosheke na ile ya mwanzo. Du´aa ya kufungulia swalah inakuwa katika ile Rak´ah ya kwanza peke yake. Ni mamoja katika swalah za faradhi na swalah zilizopendekezwa. Atasoma du´aa ya kufungulia swalah baada ya Takbiyrat-ul-Ihraam. Haikuwekwa katika Shari´ah jambo la kuikariri katika Rak´ah ya pili wala ya tatu.

Lakini baada ya kumaliza Tasliym ya kwanza na akaingia ya pili, katika Tarawiyh au swalah iliyopendekezwa, atatakiwa kusoma du´aa ya kufungulia swalah tena. Kila pale ambapo ataswali Rak´ah mbili, akasimama na kusema “Allaahu Akbar” atasoma du´aa ya kufungulia swalah. Hii ndio Sunnah katika swalah ya iliyopendekezwa na swalah ya faradhi. Kama mfano wa swalah ya Tarawiyh katika Ramadhaan au swalah ya Dhuhaa. Akiswali Rak´ah mbili au zaidi basi ataomba du´aa ya kufungulia swalah kila baada ya Rak´ah. Namna hii ndio bora.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb https://binbaz.org.sa/fatwas/14898/%D9%85%D8%B4%D8%B1%D9%88%D8%B9%D9%8A%D8%A9-%D8%AA%D9%83%D8%B1%D8%A7%D8%B1-%D8%AF%D8%B9%D8%A7%D8%A1-%D8%A7%D9%84%D8%A7%D8%B3%D8%AA%D9%81%D8%AA%D8%A7%D8%AD-%D9%81%D9%8A-%D8%B5%D9%84%D8%A7%D8%A9-%D8%A7%D9%84%D8%AA%D8%B1%D8%A7%D9%88%D9%8A%D8%AD
  • Imechapishwa: 08/05/2020