Ibn Baaz kuhusu damu ndogo na wudhuu´

Swali: Mwenye kutawadha akaumia mkono wake au mguu wake mpaka akatokwa na damu. Je, wudhuu´ wake ni wenye kuvunjika?

Jibu: Haidhuru. Damu ndogo haivunji wudhuu´. Tofauti iliyopo ni kuhusu damu nyingi ikitoka inavunja wudhuu´ au hapana. Ama kuhusu damu ndogo inayotoka mkononi au mguuni hii hakuna tofauti kwamba haivunji wudhuu´ na haidhuru.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=6898
  • Imechapishwa: 05/05/2015