Ibn Baaz kuhusu mkusanyiko wa pili msikitini

Swali: Ni ipi hukumu ya jamaa´ah inayochelewa kukaswaliwa jamaa´ah nyingine baada ya swalah ya jamaa´ah iliyoadhiniwa pamoja na imamu mteuliwa?

Jibu: Hakuna neno. Wakikuta imamu ameshaswali, waswali jamaa´ah nyingine na waswali kama jinsi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alivyoswali Jamaa´ah nyingine kwa mtu ambaye aliingia na akakuta swalah imeshampita, akawaambia baadhi ya waliokuwepo pale “Ni nani ambaye atamtolea swadaqah na kuswali naye jamaa´ah?” Kwa kuwa swalah ya watu wawili sio sawa na swalah ya mtu mmoja. Jamaa´ah ya kwanza ikimpita na akakutana na watu wengine, waswali pamoja jamaa´ah. Hili limefanya Anas na Maswahabah wengine (Radhiya Allaahu ´anhum).

Ama kauli ya wanachuoni wanaosema kuwa haitakiwi kuswali jamaa´ah [mbali na ile jamaa´ah ya kwanza], wanachotakiwa ni kurudi majumbani mwao na kuswali, hii si lolote. Ni kauli isiyokuwa na nguvu na ni dhaifu. Inaenda kinyume na Sunnah na kanuni za Kishari´ah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=6898
  • Imechapishwa: 05/05/2015