Ibn Baaz hajuzishi mtu kujitolea kiungo kumpa mgonjwa

Swali: Nilikuuliza kuhusu hukumu ya mtu kujitolea figo mbele ya Shaykh ´Abdul-´Aziyz al-Qaasim na jawabu yako ilikuwa kwamba hutoi msimamo wowote, mara nyingine – Allaah akuhifadhi – ulisema kuwa hutoi msimamo wowote na kwamba kilicho karibu zaidi na haki ni makatazo. Fatwa hii ilipelekwa shuleni ambapo mwalimu mmoja akaleta karatasi iliyo na nakala kutoka ”al-Majallatu al-´Arabiyyah”aliyoletewa na mwanafunzi mmoja ambayo ilikuwa na fatwa yako inayojuzisha mtu kujitolea figo. Je, unatupa idhini – Allaah akuhifadhi – kukusomea nayo?

Ibn Baaz: Hayo ni maoni ya baadhi ya wajumbe katika baraza.

Mwanafunzi: Ametaja kuwa imetoka kwako.

Ibn Baaz: Hata kama. Mimi najirejea ikiwa kweli imesihi kutoka kwangu.

Mwanafunzi: Nikusomee?

Ibn Baaz: Magazeti hueneza kila kitu.

Mwanafunzi: Kwa hiyo ni kipi unachothibitisha – Allaah akuhifadhi?

Ibn Baaz: Mimi naona kutofaa kujitolea kiungo. Muislamu ni mwenye kuheshimiwa ni mamoja yuko hai au ameshakufa. Hakuna chochote kinachokatwa kutoka kwake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21641/حكم-التبرع-بالكلى-واعضاء-الانسان
  • Imechapishwa: 03/09/2022