Swali: Je, inafaa kwa mwanamke kumsusa mumewe ikiwa anafanya baadhi ya madhambi kama kunywa pombe au kuzembea katika baadhi ya swalah?
Jibu: Udhahiri – na Allaah ndiye mjuzi zaidi – ni kwamba anayo haki ya kuomba talaka. Kueshi na mtu ambaye anatangaza madhambi ni maovu makubwa na khaswa inapokuja katika unywaji pombe ambapo mume anaweza kumdhuru na anaweza kumuua pasi na yeye kuhisi hilo. Kuhusu kususa kitanda asifanye hivo isipokuwa akichelea juu ya nafsi yake. Hata hivyo inafaa kwake kuomba talaka.
Kuhusu kuacha swalah ni kufuru. Hapo itamlazimu mwanamke huyo. Akiacha swalah anakufuru na hivyo itamlazimu mwanamke huyo kujitenga naye mbali na kwenda kwa familia yake kwa mujibu wa maoni sahihi. Kuiacha swalah ni ukafiri. Allaah anasema:
فَإِنْ عَلِمْتُمُوهُنَّ مُؤْمِنَاتٍ فَلَا تَرْجِعُوهُنَّ إِلَى الْكُفَّارِ ۖ لَا هُنَّ حِلٌّ لَّهُمْ وَلَا هُمْ يَحِلُّونَ لَهُنَّ
“Na mkiwatambua kuwa ni waumini basi msiwarejeshe [Makkah] kwa makafiri – wao si [wake] halali kwao [hao makafiri] na wala wao si [waume]halali kwao.”[1]
Kwa hivyo akiacha swalah ni kufuru kubwa kwa mujibu wa maoni sahihi. Katika hali hiyo itamlazimu mwanamke asimpe kitu na ajitenge naye mbali kwenda kwa familia yake mpaka atubu kwa Allaah.
Swali: Je, hili linahusiana na usiku au linakusanya usiku na mchana?
Jibu: Udhahiri ni kwamba inakusanya, lakini hiyo ni sifa ya mara nyingi. Kwa sababu mara nyingi hilo linatokea usiku. Vinginevyo inaweza kutokea katika usingizi wa mchana na inaweza kutokea katika usingizi wa asubuhi.
Swali: Vipi ikiwa anachukia tabia mbaya?
Jibu: Hapa kunahitaji upambanuzi. Ikiwa maadili yake maovu anakusudia kuwa ni mchache wa tabasamu, jambo lake ni jepesi. Lakini ikiwa maadili yake mabovu yanapelekea kumpiga, kumdhuru na kumdhulumu, basi itafaa kwake kuomba kutengana naye.
Swali: Vipi mwanamke kumsusa mumewe?
Jibu: Haifai kwake kumsusa isipokuwa kwa haki. Ni lazima kwake kumsikiliza na kumtii katika yaliyo mema. Isipokuwa asipotekeleza haki yake.
[1] 60:10
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23880/هل-للزوجة-هجر-زوجها-لاقترافه-المنكرات
- Imechapishwa: 26/05/2024
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)