Ibn Baaz akijibu baadhi ya maswali muhimu kuhusu namna ya kuswali swalah ya kupatwa kwa jua

Swali: Ni lini inaanza swalah ya kupatwa kwa jua?

Jibu: Ataanza kuswali kuanzia pale atapoona kupatwa kwa jua. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mtapoona hilo basi swalini!”

Swali: Maneno yake aliposema:

“Swalini Rak´ah mbili kwa Rukuu´ mbili.”

si kunafahamisha kuwa Rukuu´ ya pili ni ukamilifu wa Rukuu´ ya kwanza?

Jibu: Rukuu´ mbili katika kila Rak´ah. Kila Rak´ah moja inayo Rukuu´mbili, Sujuud mbili na visomo viwili. Na kila kisomo pamoja na al-Faatihah.

Swali: Je, kumepokelewa kitu kuhusu kwamba kupatwa kwa jua inatokana na madhambi?

Jibu: Imepokelewa katika Hadiyth Swahiyh ambayo amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika Khutbah yake:

“Hakuna yeyote mwenye wivu zaidi kuliko Allaah ambapo akazini mja wake au akazini mjakazi wake.”

Uzinzi ni miongoni mwa ghadhabu za Allaah (´Azza wa Jall) na ni miongoni mwa sababu za hasira pale kunapotangaa uzinzi na machafu. Tunamuomba Allaah usalama. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hakuna yeyote mwenye wivu zaidi kuliko Allaah.”

Kwa ajili hiyo akaharamisha machafu yenye kuonekana na yenye kujificha.

Swali: Je, inafaa kwake kusoma ndani ya msahafu?

Jibu: Inafaa kwake kusoma ndani ya msahafu akiwa na hifdhi. Vinginevyo asome ndani ya msahafu.

Swali: Rukuu´ ya pili ni wajibu au Sunnah?

Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alifanya hivo. Ni wajibu kufanya kama alivofanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Isitoshe amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Swalini kama mlivyoniona nikiswali.”

Swali: Je, watu wa mashambani wasiojua zaidi ya al-Faatihah wajishughulishe na kufanya Dhikr peke yake?

Jibu: Waswalini na wasome al-Faatihah na himdi zote njema anastahiki Allaah.

Swali: Je, mtu alipe Rak´ah nyingine akikosa Rukuu´ ya kwanza?

Jibu: Ndio. Akikosa Rukuu´ ya kwanza alipe Rak´ah nyingine, kwani akikosa Rukuu´ ya kwanza amekosa Rak´ah.

Swali: Baadhi ya maimamu wanategemea juu ya kuswali kwao vyombo vya khabari…

Jibu: Ni lazima kuona [kupatwa kwa mwezi]. Khabari za wahasibu hazifanyiwi kazi. Kinachotegemewa ni kuona. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mtapoona hilo basi swalini!”

Hakusema watu wakisikia au watu wakijua. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mtapoona kupatwa kwa jua.”

Kutegemea hesabu hapana.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23886/حكم-صلاة-الكسوف-وبدايتها-وكيفيتها
  • Imechapishwa: 27/05/2024