Ibn Baaz akijibu baadhi ya maswali kuhusu kuswali ndani ya msikiti wenye kaburi

Swali: Hukumu ya kuswali katika msikiti ambao kuna kaburi ndani yake au msikiti ambao katika Qiblah chake kuna kaburi lakini kuna kizuizi kama ukuta kati yao?

Jibu: Swalah ni sahihi ikiwa kaburi liko nje ya msikiti, lakini ikiwa msikiti una kaburi ndani yake, basi swalah si sahihi hata kama ni kaburi moja tu.

Swali: Je, ikiwa kaburi liko kwenye uwanja wa msikiti?

Jibu: Ikiwa uwanja huo ni sehemu ya msikiti, basi haisihi kuswali humo. Lakini ikiwa uwanja huo uko nje ya msikiti na hauhesabiki kama sehemu ya msikiti, basi hakuna tatizo.

Swali: Ikiwa kuna kizuizi, kama ukuta, baina ya kaburi na msikiti, iwe ni katika Qiblah, kulia, kushoto au nyuma ya msikiti?

Jibu: Ikiwa kaburi liko nje ya msikiti, basi swalah ni sahihi.

Swali: Ikiwa kaburi liko mashariki mwa msikiti, karibu na vyoo, na si ndani ya msikiti?

Ibn Baaz: Unakusudia nje ya msikiti.

Mwanafunzi: Ndio, nje ya msikiti.

Ibn Baaz: Haidhuru.

Swali: Ikiwa msikiti umejengwa juu ya kaburi lakini kuna kizuizi kati yao, msikiti ukatengwa na kaburi?

Jibu: Ikiwa uke nje ya msikiti na haitakiwi ndani ya msikiti kuwepo makaburi.

Swali: Lakini msikiti umejengwa juu yake?

Jibu: Kujenga misikiti juu ya makaburi… haizingatiwi kuwa umejengwa juu yake isipokuwa pale unapokuwa ndani yake.

Swali: Lakini haukujengwa isipokuwa kwa sababu yake. Kwa maana nyingine kumewekwa kaburi kisha msikiti ukaandaliwa baada yake?

Jibu: Kinachonidhihirikia ni kwamba muda wa kuwa liko nje yake basi hukumu yake… kwa ajili ya kuepuka utata inatakiwa kufukua mabaki ya kaburi na kuyahamisha makaburini. Kaburi lihamishwe na kuondoshwa.

Swali: Lakini kaburi ndio limetangulia?

Swali: Linatakiwa kuondoshwa hata kama ndio limetangulia. Linatakiwa kuondoshwa.

Swali: Ikiwa kaburi ndio limekuja baadaye?

Jibu: Linatakiwa kuondoshwa na kutengwa mbali.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24826/حكم-الصلاة-في-مسجد-في-وسطه-او-قبلته-قبر
  • Imechapishwa: 22/12/2024