Ibn Baaz akijibu baadhi ya maswali kuhusu kuligeukia jiwe jeusi

Swali: Aligeukie jiwe mwili mzima…?

Jibu: Analielekee, alielekee na kulibusu ikiwa itawezekana. Na kama akilipa upande wake na kuligusa, hakuna shida, jambo hili ni pana.

Swali: Vipi kuongeza:

بسم الله

”Kwa jina la Allaah.”?

Jibu: Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ndiye alikuwa akifanya hivo. Jambo ni lenye wasaa. Lakini sijui chochote sahihi na kuthibiti. Ni katika matendo ya Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa).

Swali: Katika mizunguko yote au mzunguko wa kwanza tu?

Jibu: Katika mizunguko yote, kuanzia wa kwanza hadi wa mwisho. Kila anapokaribia jiwe, basi alete Takbiyr kisha aendelee.

Swali: Je, kuna chochote kumepokelewa kuhusu kusujudu juu ya jiwe?

Jibu: Imepokewa katika baadhi ya Hadiyth kuhusu kusujudu juu ya jiwe. Hakuna ubaya kufanya hivyo. Kuna Hadiyth kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na zenye kuishilia kwa Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anh) kuhusu jambo hilo. Lakini Hadiyth zilizothibiti zinaeleza kuhusu kubusu. Kwa hivyo inatosha kubusu.

Swali: Kusema:

بسم الله

”Kwa jina la Allaah.”

katika mzunguko wa kwanza ni katika matendo ya Ibn ´Umar?

Jibu: Ndio, alikuwa akifanya hivyo Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh). Udhahiri ni kwamba alikuwa akifanya hivyo katika kila mzunguko. Ama Hadiyth zilizothibi zinataja tu Takbiyr.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24983ما-يصح-وما-لا-يصح-في-استقبال-الحجر-الاسود
  • Imechapishwa: 20/01/2025