Swali: Unasemaje juu ya mwenye kusema kuhusu Imaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab ya kwamba ni mjinga na sio mwanachuoni na kwamba ameweka misingi ya ujinga?

Jibu: Huyu ni mjinga wa kupindukia. Anastahiki kutiwa adabu.

Swali: Si anaritadi kwa sababu ameyaita mambo ya Tawhiyd kuwa ni ya kijinga?

Jibu: Linatakiwa kukaguliwa vyema. Kumhukumu kuwa ameritadi ni suala linatakiwa kuangaliwa vyema.

Swali: Lakini anatakiwa kushtakiwa kwa mtawala?

Jibu: Ikithibiti basi ni wajibu kwa mtawala kumtia adabu. Yote haya yanajulikana. Aliyeyasema yuko katika mji wa makafiri. Allaah atuongoze sisi na yeye. Allaah awarudishe waweze kutubia.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22928/حكم-من-يتكلم-في-الامام-محمد-بن-عبدالوهاب
  • Imechapishwa: 16/09/2023