Ibliys, Fir´awn na washirikina walilingania katika Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah?!

Msingi wa nane: Madai yake kwamba Ibliys, Fir´awn na washirikina walilingania katika Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah. al-Hajuuriy amesema katika mkanda wake “Tabyiyn al-Kadhib wal-Yamiyn”:

“Ni kweli kuwa Fir´awn na washirikina walilingania katika Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah. Haya yamesemwa pia na mwandishi wa Fath-ul-Majiyd na Ahl-us-Sunnah wote ya kwamba Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah waliilingania washirikina. Hawakuwa wanaipinga. Dalili juu ya hilo ni nyingi ya kwamba walikuwa wakilingania katika Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah.”

Sina taaliki yoyote juu ya haya. Kule tu kuyanukuu maneno haya kunatosheleza kuyaangusha.

  • Mhusika: Shaykh ´Arafaat bin Hasan bin Ja´far al-Muhammadiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Bayaan al-Fawriy (01/20-21)
  • Imechapishwa: 12/10/2016