Swali: Je, Khawaarij wanakufurisha kwa madhambi?

Jibu: Allaah ndiye mjuzi zaidi. Kinachotambulika ni kwamba wanakufurisha kwa madhambi na baadhi yao wanaonelea kuwa ni yale madhambi makubwa. Ni jambo linahitaji kulihakiki ndani ya vitabu vyao. Vitabu vyao vipo. Wana mabaki hivi sasa huko Oman, Algeria na Libyaa. Wana mabaki ambao ni Ibaadhiyyah. Hata hivyo wale waliokuja baadaye katika wao ni kana kwamba wamewepesisha baadhi ya mambo. Tumekutana na baadhi yao na hawasemi kafiri, hata hivyo wanaonelea kuwa atawekwa Motoni milele. Ni kana kwamba wameegemea zaidi katika maoni ya Mu´tazilah. Hata hivyo maana ni moja. Wakisema kuwa atawekwa Motoni milele maana yake ni kwamba amemkufurisha… kilichotangaa kutoka kwa wanazuoni ni kwamba wanasema kuwa wanakufurisha kwa madhambi kivovyote. Hata hivyo pengine wanakusudia yale madhambi yenye matishio kama vile madhambi makubwa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24326/هل-الخوارج-يكفرون-بالذنوب
  • Imechapishwa: 29/09/2024