´Ibaadah ya Mtume katika zile nyusiku kumi za mwisho Ramadhaan

795 – Mahmuud bin Ghaylaan ametuhadithia: Wakiy´ ametuhadithia: Sufyaan ametuhadithia, kutoka kwa Abu Ishaaq, kutoka kwa Hubayrah bin Yariym, kutoka kwa ´Aliy ambaye amesema:

”Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiiamsha familia yake katika zile nyusiku  kumi za mwisho za Ramadhaan.”[1]

Hadiyth ni nzuri na Swahiyh.

796- Qutaybah ametuhadithia: ´Abdul-Waahid bin Ziyaad ametuhadithia, kutoka kwa al-Hasan bin ´Ubaydillaah, kutoka kwa Ibraahiym, kutoka kwa al-Aswad, kutoka kwa ´Aaishah aliyesema:

”Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akijitahidi katika zile nyusiku kumi za mwisho kuliko anavyojitahidi katika nyusiku zengine.”[2]

Hadiyth ni nzuri, Swahiyh na geni.

[1] Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh Sunan at-Tirmidhiy” (795).

[2] Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh Sunan at-Tirmidhiy” (796).

  • Mhusika: Imaam Abu ´Iysaa Muhammad bin ´Iysaa at-Tirmidhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Jaami´ (795-796)
  • Imechapishwa: 15/05/2020