´Ibaadah haithibiti isipokuwa kwa mambo haya matatu

Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

“Kinachofuatwa katika kuthibitisha hukumu za Allaah ni Kitabu cha Allaah, Sunnah za Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na njia ya waliotangulia.”

´Ibaadah haithibiti isipokuwa kwa mambo haya:

1 – Kitabu cha Allaah, nayo ni Qur-aan tukufu.

2 – Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), au

3 – Maafikiano ya wanachuoni wa waislamu na yale waliyomo Salaf wa Ummah huu katika Maswahabah, Taabi´uun na waliokuja baada yao. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَالسَّابِقُونَ الْأَوَّلُونَ مِنَ الْمُهَاجِرِينَ وَالْأَنصَارِ وَالَّذِينَ اتَّبَعُوهُم بِإِحْسَانٍ رَّضِيَ اللَّـهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ

“Na wale waliotangulia awali [katika Uislamu] ambao ni Muhaajiruun na Answaar na wale waliowafuata kwa wema, Allaah ameridhika nao, nao wameridhika Naye.” (09:100)

Anaendelea kusema (Rahimahu Allaah):

“Haijuzu kuthibitisha hukumu ya Kishari´ah bila ya misingi hii mitatu na kunyofoa hukumu kwa hali yoyote.”

Yanayokwenda kinyume na misingi hii mitatu basi ni batili na sio sahihi kwa hali yoyote hata kama jambo hili watalipamba kwa utata, ni batili. Kwa kuwa batili haiwezi kuwa haki kamwe.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Iqtidhwaa’-is-Swiraat al-Mustaqiym (01) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/2245
  • Imechapishwa: 05/05/2015