Huyu si mfanya matabano, ni mchawi na tapeli

Swali: Ni yepi maoni yenu kuhusu imamu wa msikiti anayewasomea wagonjwa matabano, kisha huingia katika chumba nyumbani kwake na kudai kwamba anaenda Makkah ndani ya dakika chache na kwamba yeye ni miongoni mwa wale wanaokunjwa ardhi?

Jibu: Huyu ni miongoni mwa wachawi na matapeli, kwa sababu majini huwarusha baadhi ya wachawi. Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) ametaja kwamba baadhi ya wachawi hubebwa na majini siku ya ´Arafah, wakapelekwa Makkah kisha wakarudishwa. Mmoja wao hudai kwamba alikuwa pamoja na watu Makkah ilihali hakuhiji wala hakuhirimia na akarudi siku hiyohiyo. Huu ni mchezo wa mashaytwaan wanaowafanyia. Mashaytwaan wanaweza kumbeba mtu angani, wakamrusha hewani, wakampeleka ndani ya bahari au hata wakamwingiza motoni. Hivyo mtu asidanganyike na mambo hayo. Hawa ni miongoni mwa marafiki wa shaytwaan. Tunamuomba Allaah atupe usalama na afya. Haijuzu kwa mtu kutibiwa kwake na wala kuswali nyuma yake. Bali ni wajibu kutoa taarifa zake kwa watawala au kumfikisha mahakamani ili atubishwe. Akitubia, ni vyema. Asipotubia, basi atauawa. Tunamuomba Allaah atupe salama na afya.

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (24)
  • Imechapishwa: 16/09/2026