Swali: Ni ipi hukumu ya mwenye kusema:

“Kumtii mtawala ni jambo haliko katika zama zetu hizi na kwamba yeye haamini hilo na badala yake anaamini kuwa ni lazima kwa kiongozi kufuata katiba; akifuata katiba basi anafaa kutiiwa na asipoifuata hatakiwi kutiiwa?”

Jibu: Huyu anamuasi Allaah na Mtume Wake:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَأُولِي الْأَمْرِ مِنكُمْ

“Enyi mlioamini! Mtiini Allaah na mtiini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi.” (04:59)

Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayi wa sallam) anasema:

“Mwenye kumtii kiongozi basi amenitii mimi na mwenye kumuasi kiongozi ameniasi mimi.”

Haya ni madhehebu ya Khawaarij. Haya sio madhehebu ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus-ul-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/14763
  • Imechapishwa: 21/06/2020