Swali: Je, inajuzu kukaa na ambaye anawachezea shere wanachuoni, japokuwa atakuwa ni mwenye kufanya mzaha tu, ili wapate kuanasika naye au kucheka naye?

Jibu: Haya tumekwishakwambieni kwamba haifai kukaa na watu hawa. Ukikaa nao basi wewe hukumu yako ni kama yao:

وَقَدْ نَزَّلَ عَلَيْكُمْ فِي الْكِتَابِ أَنْ إِذَا سَمِعْتُمْ آيَاتِ اللَّـهِ يُكْفَرُ بِهَا وَيُسْتَهْزَأُ بِهَا فَلَا تَقْعُدُوا مَعَهُمْ حَتَّىٰ يَخُوضُوا فِي حَدِيثٍ غَيْرِهِ ۚ إِنَّكُمْ إِذًا مِّثْلُهُمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ جَامِعُ الْمُنَافِقِينَ وَالْكَافِرِينَ فِي جَهَنَّمَ جَمِيعًا

”Naye amekwishakuteremshieni katika Kitabu kwamba mnaposikia Aayah za Allaah zinakanushwa na zinafanyiwa istihzai, basi msikae pamoja nao mpaka waingie katika mazungumzo mengineyo. Vinginevyo mtakuwa kama wao. Hakika Allaah atawakusanya wanafiki na makafiri wote pamoja katika Moto wa Jahannam.” (an-Nisaa´ 04:140)

Ni mamoja mfano wao inapokuja katika kufuru au dhambi. Haijuzu kukaa katika vikao vyote vya maasi na maovu. Isipokuwa kwa njia ya kukataza na mtu akawa anajaribu kuyazuia maasi na maovu haya. Ama kukaa na wakati huohuo mtu akanyaamza, akawakunjulia kifua, kuanasika nao na kufanya nao mzaha, huyu anachukua hukumu kama wao na anakuwa mfano wao.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam (06)
  • Imechapishwa: 28/12/2018