Swali: Mimi ni mwanamke ambaye nina dhahabu ndogo nisiyoivaa. Nimeiweka kwa kuvizia siku nikitokewa na haja kubwa – Allaah asiijaalie (لا سمح الله). Nina watoto. Hujiwa na zakaah. Je, niitolee zakaah au niiuze?

Jibu: Ikiwa haijafikiwa na kile kiwango ambacho ni wajibu kutoa zakaah, ambacho ni 85 g, basi huwajibiki kutoa zakaah. Ama ikiwa imeshafikisha kile kiwango ambacho ni wajibu kutoa zakaah, basi maoni yenye nguvu ya wanachuoni ni kwamba ni wajibu kuitolea zakaah. Mtu anatakiwa kukadiria kila mwaka na atoe 2,5 %.

Kuhusu kupokea kwake zakaah kwa ajili ya matumizi yake yeye na famili yake katika vyakula, vinywaji na mavazi hakuna neno midhali ile dhahabu alionayo haizidi ile anayovaa mfano wake. Ama ikiwa inazidi basi ajitosheleze nayo na wala asipokee zakaah.

Katika swali lake ametumia neno “Allaah asijaaliie”. Anatakiwa kubadilisha badala yake atumie “Allaah asikadirie”. Kwa sababu neno “Allaah asijaalie” inamfanya mtu kufikiria kuwa Allaah anachukia jambo hili. Lakini lililo bora ni yeye kusema kwa mfano “Allaah asikadirie jambo hivo”.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (38) http://binothaimeen.net/content/875
  • Imechapishwa: 14/07/2018