Hukumu ya kwenda sehemu za pumbao za watoto

Swali: Walezi wamekuwa wakienda wao na watoto wao sehemu za pumbao. Huko kuna mambo mengi yanayoenda kinyume na Shari´ah na wanawake kuonyesha mapambo yao. Watoto wanakuwa na pupa kubwa kwenda sehemu hizi. Ni ipi hukumu ya Shari´ah ya kwenda hizo?

Jibu: Sehemu hizi za pumbao – kama alivyotaja ndugu muulizaji – kuna maovu. Sehemu kukiwa kuna maovu na ikawa mtu anaweza kuyaondosha basi italazimika kwake kwenda ili ayaondoshe. Na asipoweza itakuwa ni haramu kwake kwenda. Hivyo tunasema: toka na watoto wako kwenda nchikavu na inatosha kufanya hivo. Ama kwenda sehemu kama hizi za pumbao ilihali ndani yake kuna mchanganyiko, wapumbavu ambao wanapenda ngono na wanawake na mavazi ambayo hayafai kwa mwanamke kuyavaa si halali kwake kwenda huko. Isipokuwa akiwa ni muweza wa kuondosha maovu.

Check Also

Kuweka kompyuta na intaneti nyumbani

Swali: Ni ipi hukumu ya kuweka intaneti nyumbani, ni mamoja ikiwa kwa haja au bila …