Hukumu ya kutekeleza hukumu za Tajwiyd

Swali: Kuna watu wanamfunza mtoto wangu Qur-aan lakini hata hivyo hawamtekelezei hukumu za Tajwiyd kwa vile mwalimu ni mtumzima. Ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Hukumu za Tajwiyd sio wajibu. Zimependekezwa. Muhimu ni mtu asome kisimo kilicho wazi na azitoe zile herufi na asiangushe kitu katika herufi hizo. Kilichozidi hapo kimependekezwa na sio wajibu. Hukumu za الغنة الميم النون الساكنة zote hizi zimependekezwa. Kuhusu maneno ya al-Jizriy:

“Kuitendea kazi Tajwiyd ni lazima. Yule asiyeimairi Qur-aan anapata dhambi.”

si sahihi.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (03) http://audio2.islamweb.net/lecturs/aalrrajhee/430/430.mp3