Hukumu ya kubaki athari ya najisi baada ya kuiondosha

Swali: Mtu akifanya haja yake kisha akatawadha lakini mikononi mwake kukabaki harufu ndogo pamoja na kuwa aliosha mikono yake vizuri. Ni ipi hukumu ya swalah yake?

Jibu: Ni wajibu kuosha mikono yake vizuri. Akiiosha kwa maji inatosha. Lakini bora aioshe kwa sabuni.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (07) http://dl.islamweb.net/audiopath/audio/lecturs/aalrrajhee/434/434.mp3
  • Imechapishwa: 21/12/2018