Huku ni kumlinganisha Allaah na Mtume

Swali: Maneno ya Allaah (Ta´ala):

وَرَفَعْنَا لَكَ ذِكْرَكَ

“Tukanyanyulia juu utajo wako.” (94:04)

Katika baadhi ya misikiti kumeandikwa ifuatavyo:

“Allaah”

upande wa kulia.

“Muhammad”

upande wa kushoto.

Je, kitendo hichi kinajuzu?

Jibu: Kimekatazwa. Maana ya kitendo hichi ina maana kuwa Mtume ni sawa na Allaah (Jalla wa ´Alaa). Huku ni kumuweka sawa Mtume na Allaah. Ni muonekano mbaya. Kitendo hichi kinaweza kuzalisha I´tiqaad chafu.

Msingi kuandika msikitini kwa dhati yake ni jambo limekatazwa. Tusemeje pale ambapo jambo hilo ndani yake kutakuwa na maana mbaya? Ni wajibu kuiondosha.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (74) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1432-10-28.mp3
  • Imechapishwa: 22/08/2020