Swali: Kuna mwanamke ambaye mume wake amemhama kwa zaidi ya miaka ishirini na minane. Mwanamke huyo hamtaki mume wake na mume naye hamtaki mke wake. Kisha mume akafariki. Je, mwanamke huyo anatakiwa kukaa eda?
Jibu: Huu ni muda mrefu sana. Je, kweli huu ni uhamaji? Haijuzu kwa nuislamu kumhama ndugu yake zaidi ya siku tatu. Ikiwa alimsusa kwa sababu ya dini, basi amtendee kama Allaah alivyoamrisha:
وَاللَّاتِي تَخَافُونَ نُشُوزَهُنَّ فَعِظُوهُنَّ وَاهْجُرُوهُنَّ فِي الْمَضَاجِعِ وَاضْرِبُوهُنَّ
“Na wale ambao mnachelea uasi wao wa ndoa, basi wanasihini na wahameni katika malazi na wapigeni.”[1]
Lakini si kwa muda mrefu wa namna hii. Bali lililo wajibu ni kama Allaah (Ta´ala) alivyosema:
فَإِمْسَاكٌ بِمَعْرُوفٍ أَوْ تَسْرِيحٌ بِإِحْسَانٍ
”Hivyo kuzuia kwa mujibu wa Shari´ah au kuachia kwa wema.”[2]
Ikiwa hakumtaliki, basi atakaa eda. Wote wawili ni wenye kufanya maasi katika jambo hili. Wamehamaana, jambo ambalo halijuzu; isipokuwa ikiwa mwanamke alikuwa anafanya maasi. Hapo mume afanye kama Allaah alivyomwamrisha ikiwa mke hatimizi haki yake: amwonye, kisha amhame katika malazi, kisha ampige pigo la kumtia adabu. Ikiwa hatatengenea, basi amtaliki. Ama kuendelea kubaki katika hali ya kuhamana kwa muda wote huo, basi hilo halijuzu. Tunamuomba Allaah atupe usalama.
[1] 04:34
[2] 02:229
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (24)
- Imechapishwa: 12/09/2026
Swali: Kuna mwanamke ambaye mume wake amemhama kwa zaidi ya miaka ishirini na minane. Mwanamke huyo hamtaki mume wake na mume naye hamtaki mke wake. Kisha mume akafariki. Je, mwanamke huyo anatakiwa kukaa eda?
Jibu: Huu ni muda mrefu sana. Je, kweli huu ni uhamaji? Haijuzu kwa nuislamu kumhama ndugu yake zaidi ya siku tatu. Ikiwa alimsusa kwa sababu ya dini, basi amtendee kama Allaah alivyoamrisha:
وَاللَّاتِي تَخَافُونَ نُشُوزَهُنَّ فَعِظُوهُنَّ وَاهْجُرُوهُنَّ فِي الْمَضَاجِعِ وَاضْرِبُوهُنَّ
“Na wale ambao mnachelea uasi wao wa ndoa, basi wanasihini na wahameni katika malazi na wapigeni.”[1]
Lakini si kwa muda mrefu wa namna hii. Bali lililo wajibu ni kama Allaah (Ta´ala) alivyosema:
فَإِمْسَاكٌ بِمَعْرُوفٍ أَوْ تَسْرِيحٌ بِإِحْسَانٍ
”Hivyo kuzuia kwa mujibu wa Shari´ah au kuachia kwa wema.”[2]
Ikiwa hakumtaliki, basi atakaa eda. Wote wawili ni wenye kufanya maasi katika jambo hili. Wamehamaana, jambo ambalo halijuzu; isipokuwa ikiwa mwanamke alikuwa anafanya maasi. Hapo mume afanye kama Allaah alivyomwamrisha ikiwa mke hatimizi haki yake: amwonye, kisha amhame katika malazi, kisha ampige pigo la kumtia adabu. Ikiwa hatatengenea, basi amtaliki. Ama kuendelea kubaki katika hali ya kuhamana kwa muda wote huo, basi hilo halijuzu. Tunamuomba Allaah atupe usalama.
[1] 04:34
[2] 02:229
Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (24)
Imechapishwa: 12/09/2026
https://firqatunnajia.com/huku-kweli-ni-kumsusa-mke/