Swali: Je, mwanamke anatakiwa kumkalia eda mume wake ikiwa amefariki kabla ya kumwingilia?
Jibu: Ndiyo. Ama ikiwa amemtaliki kabla ya kumwingilia, basi hakai eda. Hilo ni kutokana na maneno Yake (Ta´ala):
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا نَكَحْتُمُ الْمُؤْمِنَاتِ ثُمَّ طَلَّقْتُمُوهُنَّ مِن قَبْلِ أَن تَمَسُّوهُنَّ فَمَا لَكُمْ عَلَيْهِنَّ مِنْ عِدَّةٍ تَعْتَدُّونَهَا
“Enyi walioamini! Mnapofunga ndoa na waumini wa kike kisha mkawataliki kabla ya kuwajamii, basi hamna juu yao eda yoyote mtakayohesabu.”[1]
Hukumu hii ni ikiwa amemtaliki. Ama kifo, basi hukumu yake ni tofauti na hilo. Hilo ni kutokana na ujumla wa maneno Yake (Ta´ala):
وَالَّذِينَ يُتَوَفَّوْنَ مِنكُمْ وَيَذَرُونَ أَزْوَاجًا يَتَرَبَّصْنَ بِأَنفُسِهِنَّ أَرْبَعَةَ أَشْهُرٍ وَعَشْرًا
“Na wale wanaofishwa miongoni mwenu na wakaacha wake, hao wake wangojee peke yao [eda ya] miezi minne na siku kumi.”[2]
Aayah hii ni ya yenye kuenea na inamuhusu mwanamke aliyeingiliwa na yule ambaye hakuingiliwa.
[1] 33:49
[2] 02:234
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (24)
- Imechapishwa: 12/09/2026
Swali: Je, mwanamke anatakiwa kumkalia eda mume wake ikiwa amefariki kabla ya kumwingilia?
Jibu: Ndiyo. Ama ikiwa amemtaliki kabla ya kumwingilia, basi hakai eda. Hilo ni kutokana na maneno Yake (Ta´ala):
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا نَكَحْتُمُ الْمُؤْمِنَاتِ ثُمَّ طَلَّقْتُمُوهُنَّ مِن قَبْلِ أَن تَمَسُّوهُنَّ فَمَا لَكُمْ عَلَيْهِنَّ مِنْ عِدَّةٍ تَعْتَدُّونَهَا
“Enyi walioamini! Mnapofunga ndoa na waumini wa kike kisha mkawataliki kabla ya kuwajamii, basi hamna juu yao eda yoyote mtakayohesabu.”[1]
Hukumu hii ni ikiwa amemtaliki. Ama kifo, basi hukumu yake ni tofauti na hilo. Hilo ni kutokana na ujumla wa maneno Yake (Ta´ala):
وَالَّذِينَ يُتَوَفَّوْنَ مِنكُمْ وَيَذَرُونَ أَزْوَاجًا يَتَرَبَّصْنَ بِأَنفُسِهِنَّ أَرْبَعَةَ أَشْهُرٍ وَعَشْرًا
“Na wale wanaofishwa miongoni mwenu na wakaacha wake, hao wake wangojee peke yao [eda ya] miezi minne na siku kumi.”[2]
Aayah hii ni ya yenye kuenea na inamuhusu mwanamke aliyeingiliwa na yule ambaye hakuingiliwa.
[1] 33:49
[2] 02:234
Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (24)
Imechapishwa: 12/09/2026
https://firqatunnajia.com/eda-ya-mwanamke-aliyekufa-mume-wake-kabla-ya-kumwingilia/