Swali: Wakati Dr. Yaasiyn Ghadhwbaan anapozungumzia Hizb-ut-Tahriyr anasema kwamba Da´wah yao haiachani na Da´wah inayopatikana katika makundi ya Kiislamu ambayo yana ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah.

Jibu: Jambo la kwanza ninamnasihi Yaasiyn Ghadhwbaan (Kukasirika) abadilishe jina, lakini pamoja na kuwa ni jina la baba yake. Kwa kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akibadilisha majina mabaya. Kadhalika imepokelewa na al-Bukhaariy kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema kwa kukariri mara tatu:

“Usikasirike!”

Isitoshe amekataza hakimu hukuhumu katika hali ya hasira, kama ambavyo alipokea al-Bukhaariy na Muslim.

Huenda unaandika kitabu chako katika hali ya hasira. Hasira imekuchukua na umeshindwa kuona tofauti kati ya Hizb-ut-Tahriyr, Ahl-us-Sunnah, al-Ikhwaan al-Muslimuun na Jamaa´at-ut-Tabliygh. Unasema kuwa wote ni Ahl-us-Sunnah. Muasisi wa Hizb-ut-Tahriyr Taqqiyy-ud-Diyn an-Naabulsiy aliulizwa kwa nini hafanyi wafuasi wake wakahifadhi Qur-aan. Jibu lake ilikuwa:

“Sitaki waje kuipa nyongo dunia.”

Da´wah yake ni kama Da´wah ya Mu´tazilah. Imejengeka juu ya matamanio na sio Qur-aan na Sunnah.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Burkaan, uk. 25-26
  • Imechapishwa: 26/08/2020