Swali: Inajuzu kupangusa juu ya Shimaagh na Ghutrah zikifungwa shingoni?

Jibu: Hapana. Sio kilemba ndio maana hafai kupangusa juu yake. Hukumu imefungamana na kile ambacho waarabu wanaita ´kilemba`. Kilemba ni kile kinakuwa kimezungushwa kichwani na kikaonekana kama mnara. Kisha ndio kikafungwa. Hiki ndio kilemba kinachopanguswa juu yake. Ama skafu, Ghutrah na Shimaagh haviitwi ´kilemba`.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (5) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdt–01041434.mp3
  • Imechapishwa: 24/10/2016