Muhammad bin Ahmad al-Haddaad amesema: Nilimsikia Mansuur al-Faqiyh akisema:

“Pindi nilipokuwa kwa Abu Zur´ah ad-Dimashqiy kulizungumzwa makhaliyfah ambapo nikauliza: “Je, inafaa mtenda dhambi kuwa wakili?” Akajibu: “Hapana.” Nikauliza: “Inafaa akawa ni msimamizi wa mwanamke?” Akajibu: “Hapana.” Nikauliza: “Inafaa akawa ni khaliyfah?” Akasema: “Ee Abul-Hasan! Haya ni maswali ya Khawaarij.”

Abu Zur´ah alikuwa akimpa dinari mia kila ambaye anahifadhi “al-Mukhtaswar” ya al-Muzaniy. Yeye ndiye ambaye aliingiza madhehebu ya ash-Shaafi´iy Dameski. Maoni yake mara nyingi yalikuwa yakiafiana na maoni ya al-Awzaa´iy.

Alikuwa ni miongoni mwa walaji na alikuwa naweza kula kikapu cha aprikoti na kikapu cha tini.

Alifariki 302 Dameski.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Siyar A´laam-in-Nubalaa’ (14/233)
  • Imechapishwa: 05/11/2020