Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

al-Bukhaariy na Muslim wamepokea kupitia kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ninatamani lau tungeliwaona ndugu zetu.” Waseme: “Ee Mtume wa Allaah! Kwani sisi sio ndugu zako?” Akasema: “Nyinyi ni Maswahabah zangu. Ndugu zangu ni wale ambao bado hawajaja.” Wakasema: “Ee Mtume wa Allaah! Vipi utamjua ni nani katika Ummah wako ambaye bado hajaja?” Akajibu: “Mnaonaje lau mtu atakuwa na farasi mwenye baka jeupe kati ya farasi weusi, hatomjua farasi wake?” Wakasema: “Ndio, ee Mtume wa Allaah.” Akasema: “Watakuja wakiwa na mabaka ya kung´aa yanayotokamana na wudhuu´. Nitawatangulia katika hodhi. Hata hivyo kuna wanamme wataofukuzwa mbali na hodhi yangu siku ya Qiyaamah kama anavyofukuzwa ngamia aliyepotea. Ninawaita, lakini kutasemwa: “Walibadilisha baada yako”, kisha niseme: “Tokomeeni! Tokomeeni!”[1]

MAELEZO

Tokomeeni – Bi maana akae mbali yule aliyeritadi baada yangu. Alama ya Ummah wake watakuwa na baka jeupe kutokamana na athari ya wudhuu´. Ummah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) walengwa ni wale walioitikia wito wake.

[1] Muslim (249).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fadhwl-il-Islaam, uk. 40-41
  • Imechapishwa: 05/11/2020