Alama ya tatu inayofahamisha Ahl-ul-Bid´ah wal-Ahwaa´ ni kufuata matamanio. Hilo limeashiriwa na Allaah (Ta´ala) pale aliposema:

فَأَمَّا الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِمْ زَيْغٌ فَيَتَّبِعُونَ مَا تَشَابَهَ مِنْهُ ابْتِغَاءَ الْفِتْنَةِ وَابْتِغَاءَ تَأْوِيلِهِ

“Ama wale ambao katika nyoyo zao mna upotovu hufuata zile [Aayah] zilizo zisizokuwa wazi kwa kutafuta fitina na kutafuta kuzipotosha.” (03:07)

Upotevu ni upindaji kutoka katika haki kwa sababu ya kufuata matamanio[1].

Mfano wa kufuata matamanio baadhi ya walinganizi katika kila zama wanaona kuwa mlinganizi anaweza kulingania katika dini ya Allaah kwa isiyokuwa njia aliyolingania kwayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah zake watukufu.

Suufiyyah wanalingania katika dini ya Allaah (Ta´ala) kwa nyimbo.

al-Ikhwaan al-Muslimuun wanaona ni sawa kulingania katika dini ya Allaah (Ta´ala) kwa filamu, maigizo, kucheza na mfano wa hayo.

Jamaa´at-ut-Tabliygh wanaona ni sawa kulingania katika dini ya Allaah (Ta´ala) kwa utokaji uliyowekewa mpaka na mfano wa hayo.

Ni jambo lisilokuwa na shaka kuwa huku ni kuyapa kipaumbele matamanio juu ya uongofu. Kuna dalili katika Shari´ah ya kwamba pale kitendo kitapokuwa hakiafikiani na Shari´ah ya Allaah kinarudishwa na hakikubaliwi.

[1] al-I´tiswaam (3/172) ya ash-Shaatwibiy.

  • Mhusika: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas Aal ´Abdil-Kariym
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Jarh wat-Ta´diyl ´indas-Salaf, uk. 62-63
  • Imechapishwa: 09/08/2020