Himdi na Tasmiyah kabla na baada ya kula

Swali: Je, mtu anatakiwa kumhimidi Allaah kabla ya Tasmiyah kabla ya chakula au ni kwa njia ya kutafuta baraka?

Jibu: Kumhimidi Allaah kunatakikana daima. Kilichowekwa katika Shari´ah ni kumtaja Allaah. Kumhimidi Allaah ni aina fulani ya Tasmiyah. Hata hivyo kilichosuniwa ni kuleta Tasmiyah kabla ya kuanza kula na kumhimidi Allaah wakati wa kumaliza. Akikusanya kati ya hayo mawili kwa namna ya kwamba akamtaja na akamhimidi Allaah wakati wa kula na akafanya vivyo hivyo baada ya kumaliza, ni kheri juu ya kheri.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24331/هل-يسن-الحمد-قبل-التسمية-على-الطعام
  • Imechapishwa: 03/10/2024